Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Aali-Imran 3:161

3:161
وما كان لنبي ان يغل ومن يغلل يات بما غل يوم القيامة ثم توفى كل نفس ما كسبت وهم لا يظلمون ١٦١
وَمَا كَانَ لِنَبِىٍّ أَن يَغُلَّ ۚ وَمَن يَغْلُلْ يَأْتِ بِمَا غَلَّ يَوْمَ ٱلْقِيَـٰمَةِ ۚ ثُمَّ تُوَفَّىٰ كُلُّ نَفْسٍۢ مَّا كَسَبَتْ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ ١٦١
وَمَا
كَانَ
لِنَبِيٍّ
أَن
يَغُلَّۚ
وَمَن
يَغۡلُلۡ
يَأۡتِ
بِمَا
غَلَّ
يَوۡمَ
ٱلۡقِيَٰمَةِۚ
ثُمَّ
تُوَفَّىٰ
كُلُّ
نَفۡسٖ
مَّا
كَسَبَتۡ
وَهُمۡ
لَا
يُظۡلَمُونَ
١٦١
Na haiwezekani kwa Nabii yeyote kufanya khiyana. Na atakaye fanya khiyana, atayaleta Siku ya Kiyama aliyo yafanyia khiyana, kisha kila mtu atalipwa kwa aliyo yachuma, kwa ukamilifu; wala hawatadhulumiwa. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Haiwi kwa Mtume kuwafanyia hiana maswahaba wake kwa kutwaa kitu katika ngawira ambayo Mwenyezi Mungu Hakumtengea. Na yoyote mwenye kulifanya hilo, miongoni mwenu, atakuja Siku ya Kiyama akiwa amekibeba kile alichokitwaa, ili afedheheshwe nacho mbele ya kila mtu katika kisimamo kinachojumuisha watu wote. Kisha itapewa kila nafsi malipo kamili ya ilichokichuma pasi na kupunguzwa wala kufanyiwa dhuluma.