Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Aali-Imran 3:17

3:17
الصابرين والصادقين والقانتين والمنفقين والمستغفرين بالاسحار ١٧
ٱلصَّـٰبِرِينَ وَٱلصَّـٰدِقِينَ وَٱلْقَـٰنِتِينَ وَٱلْمُنفِقِينَ وَٱلْمُسْتَغْفِرِينَ بِٱلْأَسْحَارِ ١٧
ٱلصَّٰبِرِينَ
وَٱلصَّٰدِقِينَ
وَٱلۡقَٰنِتِينَ
وَٱلۡمُنفِقِينَ
وَٱلۡمُسۡتَغۡفِرِينَ
بِٱلۡأَسۡحَارِ
١٧
Wanao subiri, wanao sema kweli, na wat'iifu, na wanao toa sadaka, na wanao omba maghafira kabla ya alfajiri. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Hawa ndio waliosifika kwa subira juu ya kumtii Mwenyezi Mungu, kuepuka maasia na juu ya shida zinazowafikia zilizokadiriwa na Mwenyezi Mungu. Na ndio waliosifika kwa ukweli wa maneno na vitendo na kutii kikamilifu. Na ndio waliosifika kwa utoaji, wa siri na wadhahiri, na kwa kuleta istighfar: kuomba msamaha, katika mwisho wa usiku, kwa kuwa wakati huo unatarajiwa zaidi kukubaliwa amali na kujibiwa dua.