Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Aali-Imran 3:187

3:187
واذ اخذ الله ميثاق الذين اوتوا الكتاب لتبيننه للناس ولا تكتمونه فنبذوه وراء ظهورهم واشتروا به ثمنا قليلا فبيس ما يشترون ١٨٧
وَإِذْ أَخَذَ ٱللَّهُ مِيثَـٰقَ ٱلَّذِينَ أُوتُوا۟ ٱلْكِتَـٰبَ لَتُبَيِّنُنَّهُۥ لِلنَّاسِ وَلَا تَكْتُمُونَهُۥ فَنَبَذُوهُ وَرَآءَ ظُهُورِهِمْ وَٱشْتَرَوْا۟ بِهِۦ ثَمَنًۭا قَلِيلًۭا ۖ فَبِئْسَ مَا يَشْتَرُونَ ١٨٧
وَإِذۡ
أَخَذَ
ٱللَّهُ
مِيثَٰقَ
ٱلَّذِينَ
أُوتُواْ
ٱلۡكِتَٰبَ
لَتُبَيِّنُنَّهُۥ
لِلنَّاسِ
وَلَا
تَكۡتُمُونَهُۥ
فَنَبَذُوهُ
وَرَآءَ
ظُهُورِهِمۡ
وَٱشۡتَرَوۡاْ
بِهِۦ
ثَمَنٗا
قَلِيلٗاۖ
فَبِئۡسَ
مَا
يَشۡتَرُونَ
١٨٧
Na pale Mwenyezi Mungu alipo fungamana na walio pewa Kitabu kuwa: Lazima mtawabainishia watu, wala hamtokificha, walikitupa nyuma ya migongo yao, na wakanunua kwacho thamani duni. Basi ni kiovu hicho walicho nunua. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na kumbuka, ewe Mtume, pindi Mwenyezi Mungu Alipochukua ahadi ya mkazo juu ya wale ambao Mwenyezi Mungu Amewapa Kitabu, miongoni mwa Mayahudi na Wanaswara, Mayahudi walipewa Taurati na Wanaswara walipewa Injili, ili wavitumie na wawafahamishe watu yaliyomo ndani yake wala wasiyafiche. Lakini wao waliiacha ahadi hiyo na hawakujilazimisha nayo. Na wakachukua thamni duni ikiwa ni badali ya wao kuificha haki na kukipotoa Kitabu. Ni mabaya yalioje manunuzi waliyonunua ya kuipoteza kwao ahadi na kubadilisha kwao Kitabu.