Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Aali-Imran 3:23

3:23
الم تر الى الذين اوتوا نصيبا من الكتاب يدعون الى كتاب الله ليحكم بينهم ثم يتولى فريق منهم وهم معرضون ٢٣
أَلَمْ تَرَ إِلَى ٱلَّذِينَ أُوتُوا۟ نَصِيبًۭا مِّنَ ٱلْكِتَـٰبِ يُدْعَوْنَ إِلَىٰ كِتَـٰبِ ٱللَّهِ لِيَحْكُمَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ يَتَوَلَّىٰ فَرِيقٌۭ مِّنْهُمْ وَهُم مُّعْرِضُونَ ٢٣
أَلَمۡ
تَرَ
إِلَى
ٱلَّذِينَ
أُوتُواْ
نَصِيبٗا
مِّنَ
ٱلۡكِتَٰبِ
يُدۡعَوۡنَ
إِلَىٰ
كِتَٰبِ
ٱللَّهِ
لِيَحۡكُمَ
بَيۡنَهُمۡ
ثُمَّ
يَتَوَلَّىٰ
فَرِيقٞ
مِّنۡهُمۡ
وَهُم
مُّعۡرِضُونَ
٢٣
Huwaoni wale walio pewa sehemu ya Kitabu? Wanaitwa kukiendea Kitabu cha Mwenyezi Mungu ili kiwahukumu baina yao; kisha baadhi yao wanageuka wanakikataa. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Je, umeona, ewe Mtume, hali ya kustaajabisha zaidi kuliko hali ya hawa Mayahudi, ambao Mwenyezi Mungu Amewapa fungu katika Kitabu wakajua kuwa yale uliyoyaleta ni haki, wanaitwa wafuate yaliyokuja katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu, nacho ni Qur’ani, ili kitoe uamuzi katika mambo waliotafautiana juu yake, kisha wengi wao wanakataa uamuzi huo iwapo haulingani na matamanio yao, kwa kuwa desturi yao ni ni kuipa mgongo haki?