Hayo ni kwa sababu walisema: Hautatugusa Moto isipo kuwa kwa siku chache tu. Na yakawadanganya katika dini yao yale ambayo wenyewe waliyo kuwa wakiyazua. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
kujiepusha huko na haki, sababu yake ni itikadi mbaya walionayo Watu wa Kitabu kwamba wao hawataadhibiwa isipokuwa siku chache. Itikadi hii iliwapelekea wao wamfanyiye ujasiri Mwenyezi Mungu na waidharau Dini Yake na waendelee na dini yao ya batili ambayo walijidanganya nayo nafsi zao.