Naye atazungumza na watu katika utoto wake na katika utuuzima wake, na atakuwa katika watu wema. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na atasema na watu na hali yeye ni mtoto mchanga wa kunyonya kabla hajafikia wakati wa kusema. Na atawaita wao kwa Mwenyezi Mungu, akiwa mkubwa wakati ambapo nguvu zake zitakuwa zimeshikana na ubarobaro wake umekamilika, kwa yale aliyoletewa wahyi na Mwenyezi Mungu. Kusema huku ni kuhusu utume, ulinganizi na uongozi. Na yeye anahesabiwa kuwa ni mmoja wa watu wema na wenye utukufu wa maneno na vitendo.