Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Aali-Imran 3:64

3:64
قل يا اهل الكتاب تعالوا الى كلمة سواء بيننا وبينكم الا نعبد الا الله ولا نشرك به شييا ولا يتخذ بعضنا بعضا اربابا من دون الله فان تولوا فقولوا اشهدوا بانا مسلمون ٦٤
قُلْ يَـٰٓأَهْلَ ٱلْكِتَـٰبِ تَعَالَوْا۟ إِلَىٰ كَلِمَةٍۢ سَوَآءٍۭ بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمْ أَلَّا نَعْبُدَ إِلَّا ٱللَّهَ وَلَا نُشْرِكَ بِهِۦ شَيْـًۭٔا وَلَا يَتَّخِذَ بَعْضُنَا بَعْضًا أَرْبَابًۭا مِّن دُونِ ٱللَّهِ ۚ فَإِن تَوَلَّوْا۟ فَقُولُوا۟ ٱشْهَدُوا۟ بِأَنَّا مُسْلِمُونَ ٦٤
قُلۡ
يَٰٓأَهۡلَ
ٱلۡكِتَٰبِ
تَعَالَوۡاْ
إِلَىٰ
كَلِمَةٖ
سَوَآءِۭ
بَيۡنَنَا
وَبَيۡنَكُمۡ
أَلَّا
نَعۡبُدَ
إِلَّا
ٱللَّهَ
وَلَا
نُشۡرِكَ
بِهِۦ
شَيۡـٔٗا
وَلَا
يَتَّخِذَ
بَعۡضُنَا
بَعۡضًا
أَرۡبَابٗا
مِّن
دُونِ
ٱللَّهِۚ
فَإِن
تَوَلَّوۡاْ
فَقُولُواْ
ٱشۡهَدُواْ
بِأَنَّا
مُسۡلِمُونَ
٦٤
Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Njooni kwenye neno lilio sawa baina yetu na nyinyi: Ya kwamba tusimuabudu yeyote ila Mwenyezi Mungu, wala tusimshirikishe na chochote; wala tusifanyane sisi kwa sisi kuwa Waola Walezi badala ya Mwenyezi Mungu. Na wakigeuka basi semeni: Shuhudi- eni ya kwamba sisi ni Waislamu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Sema, ewe Mtume, kuwaambia Watu wa Kitabu miongoni mwa Mayahudi na Wanaswara, «Njooni kwenye neno la uadilifu na haki tushikamane nalo sote. Nalo ni sisi kuielekeza ibada yetu kwa Mwenyezi Mungu Peke Yake. Na tusimfanye yoyote kuwa ni mshirika pamoja na Yeye, awe ni sanamu au msalaba au Shetani au kinginecho. Na wala wasiwadhalilikie baadhi yetu watu wengine kwa kuwatii badala ya Mwenyezi Mungu.» Basi wakiukataa mwito huu mzuri, waambieni wao, enyi Waumini, «Kuweni ni mashahidi kwetu kuwa sisi tumejisalimisha kwa Mola wetu na tumenyosha shingo zetu Kwake kwa kukubali kuwa ni waja Wake na kwa kumtakasa.» Na mwito huu kwenye neno la sawa, kama unavyoelekezwa kwa Mayahudi na Wanaswara, unaelekezwa pia kwa wenye mwenendo kama wao.