Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Aali-Imran 3:66

3:66
ها انتم هاولاء حاججتم فيما لكم به علم فلم تحاجون فيما ليس لكم به علم والله يعلم وانتم لا تعلمون ٦٦
هَـٰٓأَنتُمْ هَـٰٓؤُلَآءِ حَـٰجَجْتُمْ فِيمَا لَكُم بِهِۦ عِلْمٌۭ فَلِمَ تُحَآجُّونَ فِيمَا لَيْسَ لَكُم بِهِۦ عِلْمٌۭ ۚ وَٱللَّهُ يَعْلَمُ وَأَنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ ٦٦
هَٰٓأَنتُمۡ
هَٰٓؤُلَآءِ
حَٰجَجۡتُمۡ
فِيمَا
لَكُم
بِهِۦ
عِلۡمٞ
فَلِمَ
تُحَآجُّونَ
فِيمَا
لَيۡسَ
لَكُم
بِهِۦ
عِلۡمٞۚ
وَٱللَّهُ
يَعۡلَمُ
وَأَنتُمۡ
لَا
تَعۡلَمُونَ
٦٦
Angalieni! Nyinyi mlibishana katika yale mliyo yajua. Mbona sasa mnabishana katika yale msiyo yajua? Na Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye, na nyinyi hamjui. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Ndio nyinyi enyi hawa, mliomjadili Mtume wa Mwenyezi Mungu , rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, juu ya mambo ya dini yenu ambayo muna ujuzi nayo, katika yale yaliyomo ndani ya vitabu vyenu mnayoitakidi usahihi wake. Lakini ni kwa nini nyinyi mnayajadili mambo ya Ibrāhīm ambayo hamuna ujuzi nayo? Na Mwenyezi Mungu Anayajua mambo pamoja na kuwa yamefichika, na nyinyi hamjui.