Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Aali-Imran 3:78

3:78
وان منهم لفريقا يلوون السنتهم بالكتاب لتحسبوه من الكتاب وما هو من الكتاب ويقولون هو من عند الله وما هو من عند الله ويقولون على الله الكذب وهم يعلمون ٧٨
وَإِنَّ مِنْهُمْ لَفَرِيقًۭا يَلْوُۥنَ أَلْسِنَتَهُم بِٱلْكِتَـٰبِ لِتَحْسَبُوهُ مِنَ ٱلْكِتَـٰبِ وَمَا هُوَ مِنَ ٱلْكِتَـٰبِ وَيَقُولُونَ هُوَ مِنْ عِندِ ٱللَّهِ وَمَا هُوَ مِنْ عِندِ ٱللَّهِ وَيَقُولُونَ عَلَى ٱللَّهِ ٱلْكَذِبَ وَهُمْ يَعْلَمُونَ ٧٨
وَإِنَّ
مِنۡهُمۡ
لَفَرِيقٗا
يَلۡوُۥنَ
أَلۡسِنَتَهُم
بِٱلۡكِتَٰبِ
لِتَحۡسَبُوهُ
مِنَ
ٱلۡكِتَٰبِ
وَمَا
هُوَ
مِنَ
ٱلۡكِتَٰبِ
وَيَقُولُونَ
هُوَ
مِنۡ
عِندِ
ٱللَّهِ
وَمَا
هُوَ
مِنۡ
عِندِ
ٱللَّهِۖ
وَيَقُولُونَ
عَلَى
ٱللَّهِ
ٱلۡكَذِبَ
وَهُمۡ
يَعۡلَمُونَ
٧٨
Na wapo baadhi yao wanao pindua ndimi zao katika kusoma Kitabu ili mdhanie kuwa hayo yanatoka Kitabuni, na wala hayatoki Kitabuni. Na husema: Haya yametoka kwa Mwenyezi Mungu. Na wala hayatoki kwa Mwenyezi Mungu. Na wanamsingizia Mwenyezi Mungu uwongo na wao wanajua. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Miongoni mwa Mayahudi kuna watu wanaoyapotoa maneno na kuyaondoa mahali pake. Na wanayabadilisha maneno ya Mwenyezi Mungu, ili kuwafanya wasiokuwa wao wadhanie kuwa hayo ni miongoni mwa maneno yaliyoteremshwa katika Taurati, nayo si katika maneno yaliyomo kwenye Taurati kabisa, na wanasema, «Haya yanatoka kwa Mwenyezi Mungu, yameletwa kwa Nabii Wake Mūsā kwa njia ya wahyi.» Nayo hayatoki kwa Mwenyezi Mungu. Na wao, kwa ajili ya ulimwengu wao, wanasema urongo kumzulia Mwenyezi Mungu, na hali wanajua kuwa wao ni warongo.