Isipo kuwa wale walio tubu baada ya hayo na wakatengenea; kwani Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe na Mwenye kurehemu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Isipokuwa waliorudi kwa Mola wao kwa kutubia kidhati baada ya ukafiri wao na udhalimu wao na wakayatengeneza, kwa toba yao, waliyoyaharibu. Mwenyezi Mungu Ataikubali hiyo toba, kwani Yeye ni Mwingi wa kusamehe madhambi ya waja wake, ni Mwenye huruma kwao.