KABISA HAMTAFIKIA wema mpaka mtoe katika vile mnavyo vipenda. Na kitu chochote mnacho kitoa basi hakika Mwenyezi Mungu anakijua. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Hamuwezi kupata Pepo ng’o! mpaka mtoe sadaka katika vile vitu mnavyovipenda. Na chochote mnachokitoa sadaka, kiwe ni kichache au ni kingi, basi Mwenyezi Mungu Anakijua mno na Atamlipa kila mtoaji malipo yanayolingana na kitendo chake.