Juu yao zipo nguo za hariri laini za kijani kibichi, na hariri nzito ya at'ilasi. Na watavikwa vikuku vya fedha, na Mola wao Mlezi atawanywesha kinywaji safi kabisa. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Juu ya miili yao pana nguo zilizoipamba, ambazo sehemu zake za ndani kuna hariri nyembamba ya rangi ya kijani, na nje yake kuna hariri nene. Na miongoni mwa mapambo watakayovishwa ni makuku ya fedha. Na Mola wao Atawanywesha, juu ya sterehe hizo, kinywaji kisicho na uchafu wala rojo.