Akahisi kuwaogopa katika nafsi yake. Wakasema: Usiwe na khofu, nao wakambashiria kupata kijana mwenye ilimu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Alipowaona hawali aliingiwa na kicho cha kuwaogopa, na hapo wakamwambia, «Usiogope! Sisi ni wajumbe wa Mwenyezi Mungu. Na wakampa bishara kwamba mkewe Sarah atamzalia mtoto atakayekuwa ni miongoni mwa watu wanaomjua Mwenyezi Mungu na kuijua Dini Yake, naye ni Isḥāq, amani imshukie.