Akasema Firauni: Ikiwa umekuja na Ishara, basi ilete ukiwa ni katika wasemao kweli. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Fir'awn alisema kumwambia Mūsā, «Ukiwa umekuja na alama, kama unavyodai, basi niletee na uihudhurishe mbele yangu, ili madai yako yawe ya sawa na ukweli wako uthibiti, iwapo wewe ni mkweli katika madai yako kuwa wewe ni mjumbe wa Mola wa viumbe.»