Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Al-Aaraf 7:127

7:127
وقال الملا من قوم فرعون اتذر موسى وقومه ليفسدوا في الارض ويذرك والهتك قال سنقتل ابناءهم ونستحيي نساءهم وانا فوقهم قاهرون ١٢٧
وَقَالَ ٱلْمَلَأُ مِن قَوْمِ فِرْعَوْنَ أَتَذَرُ مُوسَىٰ وَقَوْمَهُۥ لِيُفْسِدُوا۟ فِى ٱلْأَرْضِ وَيَذَرَكَ وَءَالِهَتَكَ ۚ قَالَ سَنُقَتِّلُ أَبْنَآءَهُمْ وَنَسْتَحْىِۦ نِسَآءَهُمْ وَإِنَّا فَوْقَهُمْ قَـٰهِرُونَ ١٢٧
وَقَالَ
ٱلۡمَلَأُ
مِن
قَوۡمِ
فِرۡعَوۡنَ
أَتَذَرُ
مُوسَىٰ
وَقَوۡمَهُۥ
لِيُفۡسِدُواْ
فِي
ٱلۡأَرۡضِ
وَيَذَرَكَ
وَءَالِهَتَكَۚ
قَالَ
سَنُقَتِّلُ
أَبۡنَآءَهُمۡ
وَنَسۡتَحۡيِۦ
نِسَآءَهُمۡ
وَإِنَّا
فَوۡقَهُمۡ
قَٰهِرُونَ
١٢٧
Wakasema waheshimiwa wa kaumu ya Firauni: Unamuacha Musa na watu wake walete uharibifu katika nchi na wakuache wewe na miungu yako? Akasema: Tutawauwa wavulana wao, na tutawaacha hai wanawake wao. Na bila ya shaka sisi ni wenye nguvu juu yao. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Watukufu na wakubwa miongoni mwa watu wa Fir'awn walisema kumwambia Fir'awn, «Unamuacha Mūsā na watu wake, Wana wa Isrāīl, wawaharibu watu katika nchi ya Misri kwa kuwageuzia dini yao na kuwaletea ibada ya Mwenyezi Mungu Peke Yake, Asiye na mshirika, na kuacha kukuabudu wewe na kuwaabudu waungu wako?» Fir'awn akasema,»Tutawaua watoto wa kiume wa Wana wa Isrāīl, na tutawaacha watoto wao wa kike waishi ili watumike; na sisi tuko juu yao kwa nguvu za ufalme na mamlaka.»