Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Al-Aaraf 7:128

7:128
قال موسى لقومه استعينوا بالله واصبروا ان الارض لله يورثها من يشاء من عباده والعاقبة للمتقين ١٢٨
قَالَ مُوسَىٰ لِقَوْمِهِ ٱسْتَعِينُوا۟ بِٱللَّهِ وَٱصْبِرُوٓا۟ ۖ إِنَّ ٱلْأَرْضَ لِلَّهِ يُورِثُهَا مَن يَشَآءُ مِنْ عِبَادِهِۦ ۖ وَٱلْعَـٰقِبَةُ لِلْمُتَّقِينَ ١٢٨
قَالَ
مُوسَىٰ
لِقَوۡمِهِ
ٱسۡتَعِينُواْ
بِٱللَّهِ
وَٱصۡبِرُوٓاْۖ
إِنَّ
ٱلۡأَرۡضَ
لِلَّهِ
يُورِثُهَا
مَن
يَشَآءُ
مِنۡ
عِبَادِهِۦۖ
وَٱلۡعَٰقِبَةُ
لِلۡمُتَّقِينَ
١٢٨
Musa akawaambia watu wake: Ombeni msaada kwa Mwenyezi Mungu, na subirini. Hakika ardhi ni ya Mwenyezi Mungu. Naye humrithisha amtakaye katika waja wake. Na mwisho ni wa wachamngu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Akasema Mūsā kuwaambia watu wake, miongoni mwa Wana wa Isrāīl, «Takeni msaada kwa Mwenyezi Mungu Awaokoe na Fir'awn na watu wake, na subirini juu ya shida zinazowapata nyinyi na watoto wenu kutoka kwa Fir 'awn. Kwani ardhi yote ni ya Mwenyezi Mungu Anamrithisha Anayemtaka miongoni mwa waja Wake. Na mwisho mwema ni wa anyemcha Mwenyezi Mungu akafanya maamrisho Yake na akajiepusha na makatazo Yake.