Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Al-Aaraf 7:129

7:129
قالوا اوذينا من قبل ان تاتينا ومن بعد ما جيتنا قال عسى ربكم ان يهلك عدوكم ويستخلفكم في الارض فينظر كيف تعملون ١٢٩
قَالُوٓا۟ أُوذِينَا مِن قَبْلِ أَن تَأْتِيَنَا وَمِنۢ بَعْدِ مَا جِئْتَنَا ۚ قَالَ عَسَىٰ رَبُّكُمْ أَن يُهْلِكَ عَدُوَّكُمْ وَيَسْتَخْلِفَكُمْ فِى ٱلْأَرْضِ فَيَنظُرَ كَيْفَ تَعْمَلُونَ ١٢٩
قَالُوٓاْ
أُوذِينَا
مِن
قَبۡلِ
أَن
تَأۡتِيَنَا
وَمِنۢ
بَعۡدِ
مَا
جِئۡتَنَاۚ
قَالَ
عَسَىٰ
رَبُّكُمۡ
أَن
يُهۡلِكَ
عَدُوَّكُمۡ
وَيَسۡتَخۡلِفَكُمۡ
فِي
ٱلۡأَرۡضِ
فَيَنظُرَ
كَيۡفَ
تَعۡمَلُونَ
١٢٩
Wakasema: Tumeudhiwa kabla hujatufikia, na baada ya wewe kutujia! Musa akasema: Huenda Mola wenu Mlezi akamhiliki adui wenu, na akakufanyeni nyinyi ndio wa kufuatia kushika nchi, ili atazame mtavyo kuja tenda nyinyi. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Walisema watu wa Mūsā, miongoni mwa Wana wa Isrāīl, kumwambia Nabii wao Mūsā, «Tulisumbuliwa na tukaudhiwa na nguvu za Fir'awn na watu wake, kwa kuuawa watoto wetu wa kiume na kuachiliwa wanawake wetu, kabla hujatujia na baada ya kutujia.» Mūsā akawaambia, «Huenda Mola wenu Akamuangamiza adui yenu, Fir'awn na watu wake, na Awaweke nyinyi katika ardhi yao badala yao, baada ya kuangamia kwao, Aangalie namna mtakavyofanya: mtashukuru au mtakufuru?»