Lakini tukiwaondolea adhabu mpaka muda fulani wao waufikie, mara wakivunja ahadi yao. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Mwenyezi Mungu Alipowaondolea adhabu Aliyoiteremsha kwao, mpaka muda ambao hapana budi wataufikia na waadhibiwe, ambapo hapo hakutawanufaisha kule kupewa muhula kuliotangulia na kuondolewa kwao adhabu mpaka wakati wa kufika kwake, punde si punde wanarudi kuvunja ahadi waliyomuahidi Mola wao na Mūsā na wanaendelea na kudumu na ukafiri wao na upotevu wao.