Na walio zikanusha Ishara zetu na mkutano wa Akhera a'mali zao zimeharibika. Kwani watalipwa ila kwa yale waliyo kuwa wakiyatenda?. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na wale ambao walizikanusha aya za Mwenyezi Mungu, hoja Zake na kukutana na Mwenyezi Mungu huko Akhera, matendo yao mema yatapomoka kwa sababu ya kukosekana sharti yake, nayo ni kumuamini Mwenyezi Mungu na kukubali kwamba malipo Yake ni kweli. Hawatalipwa huko Akhera isipokuwa malipo ya yale ambayo walikuwa wakiyafanya ulimwenguni ya ukafiri na maasia, nayo ni kukaa milele Motoni.