Hakika wale walio muabudu ndama, itawapata ghadhabu ya Mola wao Mlezi na madhila katika maisha ya dunia. Na hivi ndivyo tunavyo walipa wazushi. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Hakika wale waliomfanya kigombe ni mungu itawapata wao ghadhabu kali kutoka kwa mola wao na unyonge katika uhai wa kilimwengu, kwa sababu ya kumkanusha kwao Mola wao. Na kama tulivyofanyia hawa, tutawafanyia wazushi wenye kuleta uzushi katika Dini ya Mwenyezi Mungu; na kila mwenye uzushi katika Dini ni mnyonge.