Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Al-Aaraf 7:161

7:161
واذ قيل لهم اسكنوا هاذه القرية وكلوا منها حيث شيتم وقولوا حطة وادخلوا الباب سجدا نغفر لكم خطيياتكم سنزيد المحسنين ١٦١
وَإِذْ قِيلَ لَهُمُ ٱسْكُنُوا۟ هَـٰذِهِ ٱلْقَرْيَةَ وَكُلُوا۟ مِنْهَا حَيْثُ شِئْتُمْ وَقُولُوا۟ حِطَّةٌۭ وَٱدْخُلُوا۟ ٱلْبَابَ سُجَّدًۭا نَّغْفِرْ لَكُمْ خَطِيٓـَٔـٰتِكُمْ ۚ سَنَزِيدُ ٱلْمُحْسِنِينَ ١٦١
وَإِذۡ
قِيلَ
لَهُمُ
ٱسۡكُنُواْ
هَٰذِهِ
ٱلۡقَرۡيَةَ
وَكُلُواْ
مِنۡهَا
حَيۡثُ
شِئۡتُمۡ
وَقُولُواْ
حِطَّةٞ
وَٱدۡخُلُواْ
ٱلۡبَابَ
سُجَّدٗا
نَّغۡفِرۡ
لَكُمۡ
خَطِيٓـَٰٔتِكُمۡۚ
سَنَزِيدُ
ٱلۡمُحۡسِنِينَ
١٦١
Na pale walipo ambiwa: Kaeni katika mji huu, na mle humo mpendapo, na semeni: Tufutie dhambi zetu. Na ingieni katika mlango wake kwa unyenyekevu, tupate kukusameheni makosa yenu. Walio wema tutawazidishia. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na kumbuka, ewe Mtume, uasi kwa Wana wa Isrāīl Mola wao, kutakata na sifa pungufu ni Kwake na kutukuka ni Kwake, na Nabii wao Mūsā, amani imshukiye, na kugeuza kwao maneno waliyoamrishwa wayaseme pindi Alipowaambia Mwenyezi Mungu, «kaeni mji wa Baitul Maqdis na kuleni matunda yake, nafaka zake na mimea yake popote mtakapo na wakati wowote mtakao na semeni, ‘tuondoshee dhambi zetu,’ na ingieni mlangoni mkimnyenyekea Mwenyezi Mungu, tutawasamehe makosa yenu na hatutawaadhibu kwayo, na tutawaongezea walio wema kheri mbili: za ulimwengu na Akhera.