Kisha nitawazukia mbele yao na nyuma yao na kuliani kwao na kushotoni kwao. Wala hutawakuta wengi wao wenye shukrani. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
«Kisha nitawajia kutoka pande zote na pambizo niwazuie wasiifuate haki, niwapambie batili, niwafanye wavutike na dunia na niwatie shaka kuhusu Akhera. Na hutawapata wengi wa wanadamu ni wenye kukushukuru wewe kwa neema zako.»