Na mkiwaita kwenye uwongofu, hawakufuateni. Ni mamoja kwenu ikiwa mtawaita au mkinyamaza. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na mnapowalingania, enyi washirikina, masanamu hawa ambao mliwaabudu badala ya Mwenyezi Mungu kwenye uongofu, hawasikii ulinganizi wenu wala hawawafuati nyinyi; inalingana sawa kuwalingania au kuwanyamazia. Kwani wao hawasikii wala hawaoni wala hawaongozi wala hawaongozwi.