Na mkiwaita kwenye uwongofu hawasikii. Na unawaona wanakutazama, nao hawaoni. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na iwapo mtawaita, enyi washirikina, hao waungu wenu kwenye kulingana sawa na haki hawatasikia mwito wenu. Na utawaona, ewe Mtume, waungu wa hawa washirikina miongoni mwa wenye kuabudu mizimu, wanakuelekea kama wanaokutazama na hali wao hawaoni kwa kuwa wao hawana macho wala busara.