Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Al-Aaraf 7:2

7:2
كتاب انزل اليك فلا يكن في صدرك حرج منه لتنذر به وذكرى للمومنين ٢
كِتَـٰبٌ أُنزِلَ إِلَيْكَ فَلَا يَكُن فِى صَدْرِكَ حَرَجٌۭ مِّنْهُ لِتُنذِرَ بِهِۦ وَذِكْرَىٰ لِلْمُؤْمِنِينَ ٢
كِتَٰبٌ
أُنزِلَ
إِلَيۡكَ
فَلَا
يَكُن
فِي
صَدۡرِكَ
حَرَجٞ
مِّنۡهُ
لِتُنذِرَ
بِهِۦ
وَذِكۡرَىٰ
لِلۡمُؤۡمِنِينَ
٢
Kitabu kilicho teremshwa kwako - basi isiwe dhiki kifuani kwako kwa ajili yake, upate kuonya kwacho, na kiwe ni ukumbusho kwa Waumini. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Hii Qur’ani ni Kitabu kitukufu, Mwenyezi Mungu Amekiteremsha kwako, ewe Mtume. Basi pasiwe na shaka katika kifua chako kwamaba imeteremshwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Na usiwe na wasiwasi katika kuifikisha kwa watu na kuwaonya nayo. Tumeiteremsha kwako ili uwatishe nayo makafiri na uwakumbushe Waumini.