Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Al-Aaraf 7:23

7:23
قالا ربنا ظلمنا انفسنا وان لم تغفر لنا وترحمنا لنكونن من الخاسرين ٢٣
قَالَا رَبَّنَا ظَلَمْنَآ أَنفُسَنَا وَإِن لَّمْ تَغْفِرْ لَنَا وَتَرْحَمْنَا لَنَكُونَنَّ مِنَ ٱلْخَـٰسِرِينَ ٢٣
قَالَا
رَبَّنَا
ظَلَمۡنَآ
أَنفُسَنَا
وَإِن
لَّمۡ
تَغۡفِرۡ
لَنَا
وَتَرۡحَمۡنَا
لَنَكُونَنَّ
مِنَ
ٱلۡخَٰسِرِينَ
٢٣
Wakasema: Mola wetu Mlezi! tumejidhulumu nafsi zetu, na kama hutusamehe na kuturehemu, hakika tutakuwa katika wenye kukhasirika. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Ādam na Ḥawwā’ walisema, «Ewe Mola wetu, tumejidhulumu nafsi zetu kwa kula kutoka kwenye mti ule. Na iwapo hutatusamehe na kuturehemu, tutakuwa ni miongoni mwa waliopoteza bahati zao katiku ulimengu wao na Akhera yao.» Maneno haya ndiyo yale aliyoyapokea Ādam kutoka kwa Mola wake akayatumia katika kumuomba, ndipo Mola wake Akaikubali toba yake.