Fuateni mliyo teremshiwa kutoka kwa Mola Mlezi wenu, wala msifuate rafiki au walinzi wengine badala yake. Ni machache mnayo yakumbuka. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Yafuateni, enyi watu, hayo yaliyoteremshwa kutoka kwa Mola wenu miongoni mwa Qur’ani na Sunnah(mafundisho ya Mtume) kwa kufuata maamrisho na kuepuka makatazo Na wala msiwafuate wategemewa badala ya Mwenyezi Mungu, kama mashetani na wasomi wa Kiyahudi na watawa wa Kinaswara. Hakika nyinyi ni mara chache mnapowaidhika na kuzingatia na mkarudi kwenye haki.