Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Al-Aaraf 7:33

7:33
قل انما حرم ربي الفواحش ما ظهر منها وما بطن والاثم والبغي بغير الحق وان تشركوا بالله ما لم ينزل به سلطانا وان تقولوا على الله ما لا تعلمون ٣٣
قُلْ إِنَّمَا حَرَّمَ رَبِّىَ ٱلْفَوَٰحِشَ مَا ظَهَرَ مِنْهَا وَمَا بَطَنَ وَٱلْإِثْمَ وَٱلْبَغْىَ بِغَيْرِ ٱلْحَقِّ وَأَن تُشْرِكُوا۟ بِٱللَّهِ مَا لَمْ يُنَزِّلْ بِهِۦ سُلْطَـٰنًۭا وَأَن تَقُولُوا۟ عَلَى ٱللَّهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ ٣٣
قُلۡ
إِنَّمَا
حَرَّمَ
رَبِّيَ
ٱلۡفَوَٰحِشَ
مَا
ظَهَرَ
مِنۡهَا
وَمَا
بَطَنَ
وَٱلۡإِثۡمَ
وَٱلۡبَغۡيَ
بِغَيۡرِ
ٱلۡحَقِّ
وَأَن
تُشۡرِكُواْ
بِٱللَّهِ
مَا
لَمۡ
يُنَزِّلۡ
بِهِۦ
سُلۡطَٰنٗا
وَأَن
تَقُولُواْ
عَلَى
ٱللَّهِ
مَا
لَا
تَعۡلَمُونَ
٣٣
Sema: Mola Mlezi wangu ameharimisha mambo machafu ya dhaahiri na ya siri, na dhambi, na uasi bila ya haki, na kumshirikisha Mwenyezi Mungu na asicho kiletea uthibitisho, na kumzulia Mwenyezi Mungu msiyo yajua. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Sema,ewe Mtume, kuwaambia washirikina hawa, «Hakika Mwenyezi Mungu Ndiye Aliyeyafanya matendo maovu kuwa ni haramu, yale yaliyo waziwazi na yale yaliyofichika, na Ameyakataza maasia yote, na miongoni mwa makubwa zaidi ya maasia ni kuwafanyia watu uadui, kwani hilo liko kando na haki. Na Amewaharamishia kuabudu, pamoja na Mwenyezi Mungu, Aliyetuka, vitu vyingine kati ya vile ambavyo Hakuviteremshia ushahidi wala hoja, kwani afanyaye hayo hana kithibitisho chochote. Na Amewaharamishia kumnasibishia Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, sheria ambayo Hakuipasisha kwa kumzulia urongo,» kama madai ya kwamba Mwenyezi Mungu Ana mwana na kuharamisha baadhi ya vilivyo halali katika mavazi na chakula.