Na wa mwanzo wao watawaambia wa mwisho wao: Basi nyinyi pia hamkuwa na ubora kuliko sisi. Basi onjeni adhabu kwa sababu ya mliyo kuwa mkiyachuma 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Hapo watasema wale waliofuatwa miongoni mwa viongozi na wengineo kuwaambia wafuasi wao, «Sisi na nyinyi tuko sawa katika uharibifu na upotevu na katika kufanya vitendo ambavyo ndio sababu ya kupata adhabu, kwa hivyo, nyinyi hamuna ubora juu yetu.» Mwenyezi Mungu Atawaambia wao wote, «Basi ionjeni adhabu,» yaani adhabu ya Jahanamu «kwa makosa mliyoyatenda.»