Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Al-Aaraf 7:4

7:4
وكم من قرية اهلكناها فجاءها باسنا بياتا او هم قايلون ٤
وَكَم مِّن قَرْيَةٍ أَهْلَكْنَـٰهَا فَجَآءَهَا بَأْسُنَا بَيَـٰتًا أَوْ هُمْ قَآئِلُونَ ٤
وَكَم
مِّن
قَرۡيَةٍ
أَهۡلَكۡنَٰهَا
فَجَآءَهَا
بَأۡسُنَا
بَيَٰتًا
أَوۡ
هُمۡ
قَآئِلُونَ
٤
Na miji mingapi tuliiangamiza, ikaifikia adhabu yetu usiku au walipo kuwa wamelala adhuhuri. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na miji mingi tuliwaangamiza watu wake kwa sababu ya kwenda kinyume kwao na Mitume wetu na kuwakanusha. Hilo likawaletea utwevu wa duniani uliounganishwa na unyonge wa Akhera. Basi adhabu yetu iliwajia, wakati mwingine wakiwa wamelala usiku, na wakati mwingine wakiwa wamelala mchana. Mwenyezi Mungu Amezihusu nyakati mbili hizi kwa kuwa ni nyakati za utulivu na mapumziko. Hivyo basi, kuja kwa adhabu kwenye nyakati mbili hizi kunababaisha zaidi na adhabu yenyewe huwa ni kali zaidi.