Jahannamu itakuwa kitanda chao na juu yao nguo za moto za kujifunika. Na hivi ndivyo tunavyo walipa madhaalimu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Makafiri hawa ni wenye kukalishwa milele Motoni. Watapata humo kwenye Moto wa Jahanamu tandiko chini yao, na juu yao kutakuwa na mifiniko inayowafinika. Na mfano wa mateso haya mabaya Atawatesa nayo Mwenyezi Mungu wale madhalimu ambao wamekiuka mipaka Yake, wakamkanusha na wakamuasi.