Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Al-Aaraf 7:56

7:56
ولا تفسدوا في الارض بعد اصلاحها وادعوه خوفا وطمعا ان رحمت الله قريب من المحسنين ٥٦
وَلَا تُفْسِدُوا۟ فِى ٱلْأَرْضِ بَعْدَ إِصْلَـٰحِهَا وَٱدْعُوهُ خَوْفًۭا وَطَمَعًا ۚ إِنَّ رَحْمَتَ ٱللَّهِ قَرِيبٌۭ مِّنَ ٱلْمُحْسِنِينَ ٥٦
وَلَا
تُفۡسِدُواْ
فِي
ٱلۡأَرۡضِ
بَعۡدَ
إِصۡلَٰحِهَا
وَٱدۡعُوهُ
خَوۡفٗا
وَطَمَعًاۚ
إِنَّ
رَحۡمَتَ
ٱللَّهِ
قَرِيبٞ
مِّنَ
ٱلۡمُحۡسِنِينَ
٥٦
Wala msifanye uharibifu katika nchi baada ya kuwa imekwisha tengenezwa. Na muombeni kwa kuogopa na kwa kutumai. Hakika rehema ya Mwenyzi Mungu iko karibu na wanao fanya mema. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Wala msilete katika ardhi aina yoyote ya uharibifu, baada ya Mwenyezi Mungu kuitengeneza kwa kutuma Mitume, amani iwashukie, na kuimarika kwa utiifu wa Mwenyezi Mungu. Na muombeni Yeye, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, mkimtakasia maombi yenu, kwa kuogopa mateso Yake na kuwa na matumaini kupata malipo Yake mazuri. Hakika rehema ya Mwenyezi Mungu iko karibu na wenye kufanya wema.