Wakasema: Je! Umetujia ili tumuabudu Mwenyezi Mungu peke yake, na tuyaache waliyo kuwa wakiyaabudu baba zetu? Basi tuletee hayo unayo tuahidi, ukiwa miongoni mwa wasemao kweli. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
’Ād walisema kumwambia Hūd, amani imshukie, «Je, umetuita tumuabudu Mwenyezi Mungu, Peke Yake, na tuihame ibada ya masanamu ambayo tumeirithi kutoka kwa mababa zetu? Basi tuletee adhabu ambayo unatutusha nayo iwapo wewe ni miongoni mwa wakweli katika hayo usemayo.»