Akasema: Hakika ujuzi uko kwa Mwenyezi Mungu. Mimi nakufikishieni niliyo tumwa. Lakini nakuoneni kuwa nyinyi mnafanya ujinga. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Hūd, amani imshukie, akasema, “Hakika ujuzi wa adhabu mliyoahidiwa uko kwa Mwenyezi Mwenyezi Mungu, na kwa kweli mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu, ninawafikishia ujumbe Alionituma nao, na lakini mimi ninawaona kuwa ni watu mlio wajinga kwa kuifanyia haraka adhabu na kuwa na ujasiri juu ya Mwenyezi Mungu.