Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Al-Ahzab 33:1

33:1
يا ايها النبي اتق الله ولا تطع الكافرين والمنافقين ان الله كان عليما حكيما ١
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّبِىُّ ٱتَّقِ ٱللَّهَ وَلَا تُطِعِ ٱلْكَـٰفِرِينَ وَٱلْمُنَـٰفِقِينَ ۗ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَلِيمًا حَكِيمًۭا ١
يَٰٓأَيُّهَا
ٱلنَّبِيُّ
ٱتَّقِ
ٱللَّهَ
وَلَا
تُطِعِ
ٱلۡكَٰفِرِينَ
وَٱلۡمُنَٰفِقِينَۚ
إِنَّ
ٱللَّهَ
كَانَ
عَلِيمًا
حَكِيمٗا
١
Ewe Nabii! Mche Mwenyezi Mungu wala usiwat'ii makafiri na wanaafiki. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye hikima. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Ewe Nabii! Endelea daima kwenye kumcha Mwenyezi Mungu kwa kuyafanya maamrisho Yake na kujiepusha na makatazo Yake, na waumini wakufuate kwa kuwa wao wanahitajia hilo zaidi kuliko wewe, na usiwatii makafiri na watu wa unafiki. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu, ni Mwenye hekima katika uumbaji Wake, amri Zake na uendeshaji mambo Wake.