Na Mwenyezi Mungu aliwarudisha nyuma makafiri juu ya ghadhabu yao; hawakupata kheri yoyote. Na Mwenyezi Mungu amewatosheleza Waumini katika vita. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na uweza. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na Akayarudisha Mwenyezi Mungu mapote ya ukafiri kutoka Madina yakiwa yamepita patupu, yamepata hasara na yamejawa na hasira, hayakupata kheri yoyote duniani wala Akhera, na Mwenyezi Mungu Akawatosheleza Waumini (wasilazimike) kupigana kwa kuwasaidia kwa sababu Alizowatolea. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Hashindwi wala Halazimishwi, ni Mshindi katika ufalme Wake na mamlaka Yake.