Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Al-Ahzab 33:32

33:32
يا نساء النبي لستن كاحد من النساء ان اتقيتن فلا تخضعن بالقول فيطمع الذي في قلبه مرض وقلن قولا معروفا ٣٢
يَـٰنِسَآءَ ٱلنَّبِىِّ لَسْتُنَّ كَأَحَدٍۢ مِّنَ ٱلنِّسَآءِ ۚ إِنِ ٱتَّقَيْتُنَّ فَلَا تَخْضَعْنَ بِٱلْقَوْلِ فَيَطْمَعَ ٱلَّذِى فِى قَلْبِهِۦ مَرَضٌۭ وَقُلْنَ قَوْلًۭا مَّعْرُوفًۭا ٣٢
يَٰنِسَآءَ
ٱلنَّبِيِّ
لَسۡتُنَّ
كَأَحَدٖ
مِّنَ
ٱلنِّسَآءِ
إِنِ
ٱتَّقَيۡتُنَّۚ
فَلَا
تَخۡضَعۡنَ
بِٱلۡقَوۡلِ
فَيَطۡمَعَ
ٱلَّذِي
فِي
قَلۡبِهِۦ
مَرَضٞ
وَقُلۡنَ
قَوۡلٗا
مَّعۡرُوفٗا
٣٢
Enyi wake wa Nabii! Nyinyi si kama yeyote katika wanawake wengine. Kama mnamcha Mungu basi msiregeze sauti zenu, akaingia tamaa mwenye maradhi katika moyo wake. Na semeni maneno mema. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Enyi wake wa Nabii! Nyinyi, katika utukufu na cheo, si kama wanawake wasiokuwa nyinyi iwapo mtafanya matendo ya utiifu kwa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na mtajiepusha na mambo ya kumuasi yeye. Basi msizungumze na wanaume wa kando kwa sauti nyororo yenye kumtia tamaa mwanamume ambaye kuna ubaya ndani ya moyo wake na ugonjwa wa kutamani haramu, (Hii ni adabu ya lazima kwa kila mwanamke Anayemuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho.) na semeni maneno yaliyo mbali na shaka yasiyokatazwa na Sheria.