Wala usiwat'ii makafiri na wanaafiki, na usijali udhia wao. Nawe mtegemee Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa Mtegemewa. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na usilitii, ewe Nabii, neno la kafiri au mnafiki na uuache udhia wao, na hilo lisikuzuie kufikisha ujumbe, na kuwa na imani na Mwenyezi Mungu katika mambo yako yote, na umtegemee Yeye, kwani Yeye Atakutosheleza yanayokutia hamu miongoni mwa mambo yote ya ulimwengu na Akhera.