Na wale wanao waudhi Waumini wanaume na wanawake pasina wao kufanya kosa lolote, bila ya shaka wamebeba dhulma kubwa na dhambi zilio dhaahiri. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na wale wenye kuwaudhi Waumini wa kiume na Waumini wa kike kwa maneno au vitendo bila ya kosa walilolifanya, basi watakuwa wametenda tendo la urongo na uzushi mbaya kabisa, na wamefanya kosa chafu waziwazi, ambalo kwalo watastahili kupewa adhabu huko Akhera.