Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Al-Ahzab 33:9

33:9
يا ايها الذين امنوا اذكروا نعمة الله عليكم اذ جاءتكم جنود فارسلنا عليهم ريحا وجنودا لم تروها وكان الله بما تعملون بصيرا ٩
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ ٱذْكُرُوا۟ نِعْمَةَ ٱللَّهِ عَلَيْكُمْ إِذْ جَآءَتْكُمْ جُنُودٌۭ فَأَرْسَلْنَا عَلَيْهِمْ رِيحًۭا وَجُنُودًۭا لَّمْ تَرَوْهَا ۚ وَكَانَ ٱللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرًا ٩
يَٰٓأَيُّهَا
ٱلَّذِينَ
ءَامَنُواْ
ٱذۡكُرُواْ
نِعۡمَةَ
ٱللَّهِ
عَلَيۡكُمۡ
إِذۡ
جَآءَتۡكُمۡ
جُنُودٞ
فَأَرۡسَلۡنَا
عَلَيۡهِمۡ
رِيحٗا
وَجُنُودٗا
لَّمۡ
تَرَوۡهَاۚ
وَكَانَ
ٱللَّهُ
بِمَا
تَعۡمَلُونَ
بَصِيرًا
٩
Enyi mlio amini! Zikumbukeni neema za Mwenyezi Mungu zilio juu yenu. Pale yalipo kufikilieni majeshi, nasi tukayapelekea upepo, na majeshi msiyo yaona. Na Mwenyezi Mungu anayaona mnayo yatenda. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Enyi Waumini! Ikumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Aliyowaneemesha nyinyi katika Madina siku ya vita vya Makundi (Aḥzāb), navyo ndivyo vita vya Shimo (Khandaq), walipojikusanya dhidi yenu washirikina kutoka nje ya Madina, na Mayahudi na wanafiki wakiwa ndani ya Madina na pambizoni mwake, wakawaviringa nyinyi, hapo tukayatumia yale makundi upepo mkali uliong’oa mahema yao na kuvirusha vyungu vyao, na tukawatumia Malaika kutoka mbinguni msiowaona, hapo basi nyoyo zao zikaingia kicho. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyaona mnayoyatenda, hakuna chochote kinachofichamana kwake katika hayo.