Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu aliye umba mbingu na ardhi, na akafanya giza na mwangaza. Tena baada ya haya walio kufuru wanawafanya wengine sawa na Mola wao Mlezi. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mwenye sifa ambazo zote ni sifa za ukamilifu, Mwenye neema za nje na za ndani, za kidini na za kidunia, Ambaye Aliumba mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake, Aliumba giza na mwangaza kwa kupishana usiku na mchana. Katika hili pana ishara ya utukufu wa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, na kuwa Yeye Peke Yake Anastahiki kuabudiwa. Haifai kwa yoyote kumshirikisha mwengine na Yeye. Na pamoja na uwazi huu, makafiri wanamsawazisha mwingine na Mwenyezi Mungu na wanamshirikisha na Yeye.