Na hakika Mitume walio kabla yako walifanyiwa kejeli, lakini walio wafanyia kejeli wakaja kuzungukwa na yale yale waliyo kuwa wao wanayafanyia kejeli. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na kwa kuwa kutaka kwao kuteremshwa Malaika kulikuwa ni kwa njia ya kumfanyia shere Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, Mwenyeyezi Mungu, Aliyetukuka, Aliwaelezea kwamba kuwafanyia shere Mitume, amani iwashukie, si jambo jipya; kwani jambo hilo lilitukia kwa makafiri waliopita kuwafanyia Mitume wao, wakazungukwa na adhabu ambayo walikuwa wakiifanyia shere na wakipinga kuja kwake.