Huyo ndiye Allah, Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wenu, hapana mungu ila Yeye, Muumba wa kila kitu. Basi muabuduni Yeye tu. Naye ni Mtegemewa wa kila kitu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Huyo, enyi washirikina, Ndiye Mola wenu, Aliyeshinda na kutukuka; hapana Mwenye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Yeye; Mwenye kuumba kila kitu. Basi mwandameni na mumnyenyekee kwa kumtii na kumuabudu. Na Yeye, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake, ni Mtegemewa na ni Mtunzi, Anayaendesha mambo ya viumbe vyake.