Nasi twazigeuza nyoyo zao na macho yao. Kama walivyo kuwa hawakuamini mara ya kwanza, tunawaacha katika maasi yao wakitangatanga. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na tutazigeuza nyoyo zao na macho yao, tuweke kizuizi baina yake na kunufaika na alama za Mwenyezi mungu, wasiziamini kama walivyokuwa hawakuziamini aya za Qur’ani zilipoteremka kwa mara ya kwanza, na tutawaacha wao wameduwaa katika kumuasi kwao Mwenyezi Mungu, hawaongoki kwenye haki na usawa.