Kadhaalika katika kila mji tumewajaalia wakubwa wa wakosefu wao wafanye vitimbi ndani yake. Na wala hawafanyii vitimbi isipo kuwa nafsi zao, nao hawatambui. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na mfano huu uliopatikana kwa viongozi wa makafiri huko Maka wa kuzuia dini ya Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, tumeweka katika kila mji watu waovu wanaongozwa na wakubwa wao, ili wapate kufanya vitimbi humo kwa kuzuia dini ya Mwenyezi Mungu; na wao hawazifanyii vitimbi isipokuwa nafsi zao, na wala hawalihisi hilo.