Hao watapata nyumba ya salama kwa Mola Mlezi wao. Naye ndiye Rafiki Mlinzi wao kwa sababu ya waliyo kuwa wakiyatenda. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Wale wanaokumbuka watapata mbele ya Mola wao, Aliyetukuka na kuwa juu, Siku ya Kiyama Nyumba ya Salama na Amani, isiyo na makero, nayo ni Pepo. Na yeye, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, ni Mwenye kuwanusuru na kuwalinda; hayo yakiwa ni malipo kwao kwa matendo yao mema.