Na wote wana daraja mbali mbali kutokana na yale waliyo yatenda. Na Mola wako Mlezi si mwenye kughafilika na yale wanayo yatenda. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na kila mwenye kufanya vitendo vya kumtii Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, vya kumuasi ana daraja kutokana na vitendo vyake, Mwenyezi Mungu Atamfikishia viwango hivyo na Atamlipa kwavyo. Na Mola wako, ewe Mtume, Hakuwa ni Mwenye kughafilika na wanayoyafanya waja Wake.