Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Al-An-Am 6:133

6:133
وربك الغني ذو الرحمة ان يشا يذهبكم ويستخلف من بعدكم ما يشاء كما انشاكم من ذرية قوم اخرين ١٣٣
وَرَبُّكَ ٱلْغَنِىُّ ذُو ٱلرَّحْمَةِ ۚ إِن يَشَأْ يُذْهِبْكُمْ وَيَسْتَخْلِفْ مِنۢ بَعْدِكُم مَّا يَشَآءُ كَمَآ أَنشَأَكُم مِّن ذُرِّيَّةِ قَوْمٍ ءَاخَرِينَ ١٣٣
وَرَبُّكَ
ٱلۡغَنِيُّ
ذُو
ٱلرَّحۡمَةِۚ
إِن
يَشَأۡ
يُذۡهِبۡكُمۡ
وَيَسۡتَخۡلِفۡ
مِنۢ
بَعۡدِكُم
مَّا
يَشَآءُ
كَمَآ
أَنشَأَكُم
مِّن
ذُرِّيَّةِ
قَوۡمٍ
ءَاخَرِينَ
١٣٣
Na Mola wako Mlezi ndiye Mkwasi, Mwenye rehema. Akipenda atakuondoeni na awaweke wengine awapendao badala yenu, kama vile alivyo kutoeni kutokana na uzazi wa watu wengine. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na Mola wako, ewe Mtume, Aliyewaamrisha watu kumuabudu, Ndiye Mkwasi Peke Yake, na viumbe wote wanamhitajia Yeye. Na Yeye, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, Ndiye Mwenye rehema kunjufu. Na lau Alitaka Angaliwaangamiza na Akawaleta watu wengine wasiokuwa nyinyi watakaokuwa badala yenu baada ya kumalizika kwenu na watende matendo ya kumtii Yeye, Aliyetukuka, kama Alivyowaleta nyinyi kutokamana na kizazi cha watu wengine waliokuwako kabla yenu.