Sema: Je, nimchukue rafiki mlinzi asiye kuwa Mwenyezi Mungu, ambaye ndiye Muumba mbingu na ardhi, naye ndiye anaye lisha wala halishwi? Sema: Mimi nimeamrishwa niwe wa kwanza wa wenye kusilimu. Na wala kabisa usiwe miongoni wa washirikina. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Sema, ewe Mtume, kuwaambia hawa wanaomshirikisha Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, na asiyekuwa Yeye, «Je, nimchukue asiyekuwa Mwenyezi Mungu kuwa ni msaidizi na ni mwokozi, na hali Yeye ni Muumba mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake, na Yeye Ndiye Mwenye kuwaruzuku viumbe Wake na hakuna mwenye kumruzuku Yeye?» Sema,ewe Mtume, «Mimi nimeamrishwa niwe ni wa mwanzo aliyemnyenyekea Yeye na kumwandama katiika umma huu. Na nimekatazwa kuwa ni miongoni mwa wanaomshirikisha Yeye na asiyekuwa Yeye.