Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Al-An-Am 6:142

6:142
ومن الانعام حمولة وفرشا كلوا مما رزقكم الله ولا تتبعوا خطوات الشيطان انه لكم عدو مبين ١٤٢
وَمِنَ ٱلْأَنْعَـٰمِ حَمُولَةًۭ وَفَرْشًۭا ۚ كُلُوا۟ مِمَّا رَزَقَكُمُ ٱللَّهُ وَلَا تَتَّبِعُوا۟ خُطُوَٰتِ ٱلشَّيْطَـٰنِ ۚ إِنَّهُۥ لَكُمْ عَدُوٌّۭ مُّبِينٌۭ ١٤٢
وَمِنَ
ٱلۡأَنۡعَٰمِ
حَمُولَةٗ
وَفَرۡشٗاۚ
كُلُواْ
مِمَّا
رَزَقَكُمُ
ٱللَّهُ
وَلَا
تَتَّبِعُواْ
خُطُوَٰتِ
ٱلشَّيۡطَٰنِۚ
إِنَّهُۥ
لَكُمۡ
عَدُوّٞ
مُّبِينٞ
١٤٢
Na katika wanyama amekujaalieni wenye kubeba mizigo na kutoa matandiko. Kuleni katika alivyo kuruzukuni Mwenyezi Mungu, wala msifuate nyayo za Shet'ani. Hakika yeye ni adui yenu dhaahiri. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na Ameleta katika wanyama wale ambao wametayarishwa kwa kubebeshwa kwa kuwa ni wakubwa na ni warefu, kama ngamia. Na miongoni mwao kuna waliotayarishwa si kwa kubebeshwa kwa kuwa ni wadogo na wafupi, kama ng’ombe, mbuzi na kondoo. Kuleni wale Aliyowahalalishia nyinyi Mwenyezi Mungu miongoni mwa hawa wanyama, wala msiwaharamishe wale Aliyowahalalisha miongoni mwao kwa kufuata njia za Shetani kama walivyofanya washirikina. Hakika Shetani, kwenu nyinyi, ni adui mwenye uadui wa wazi.